Jinsi ya Kutuma Maombi ya Diploma ya Famasi Kupitia Mfumo wa CAS – NACTVET

Admin

Mfumo wa CAS (Central Admission System) unaosimamiwa na NACTVET hutumika na waombaji wanaotaka kujiunga na vyuo vya afya, mafundi sanifu, ualimu wa diploma, n.k. kwa ngazi ya Certificate (Astashahada) na Diploma (Stashahada).

1. Tembelea Tovuti Rasmi ya CAS – NACTVET

2. Bonyeza Sehemu ya “Start Application” au “New Applicant”

  • Kwa mara ya kwanza, jisajili kwa kutumia:
    • Jina lako kamili
    • Email ya kuaminika
    • Namba ya simu
    • Nambari ya mtihani wa NECTA (CSEE)
  • Baada ya kujisajili, utapata jina la mtumiaji (username) na neno la siri (password)

3. Ingia kwenye Akaunti Yako

  • Tumia username na password kuingia kwenye akaunti
  • Mfumo utaonesha taarifa zako za NECTA (kwa waliomaliza kidato cha nne)
  • Hakikisha taarifa zote ni sahihi

4. Chagua Kozi ya Kuomba – Diploma ya Famasi

  • Katika menyu ya kozi, tafuta “Diploma in Pharmaceutical Sciences”
  • Chagua chuo/vyuo vinavyotoa kozi hiyo
    • Unaweza kuchagua hadi vyuo vitano (5) tofauti

5. Jaza Taarifa Zilizobaki

  • Taarifa binafsi: tarehe ya kuzaliwa, makazi, jinsia
  • Pakia picha ya pasipoti (passport size)
  • Hakikisha kila sehemu umejaza ipasavyo

6. Lipa Ada ya Maombi (Application Fee)

  • Ada ni TSh 10,000
  • Mfumo utakupa control number
  • Lipa kupitia:
    • M-Pesa / Tigo Pesa / Airtel Money
    • Benki ya NMB, CRDB, au benki nyingine

Mfano wa Kulipa kwa M-Pesa:

Piga *150*00# → LIPA kwa M-Pesa → Malipo ya Serikali → Ingiza control number → Kiasi → Namba ya siri

7. Thibitisha na Tuma Maombi

  • Baada ya kulipa, nenda tena kwenye akaunti yako ya CAS
  • Hakikisha taarifa zote ni sahihi
  • Thibitisha (Submit) maombi yako

8. Subiri Majibu ya Uchaguzi

  • Orodha ya waliochaguliwa hutangazwa kupitia:
    • Akaunti yako ya CAS
    • Tovuti ya NACTVET
    • Simu (SMS) au barua pepe
  • Ukichaguliwa, utapata Joining Instructions kutoka chuo husika

Mambo Muhimu ya Kukumbuka

KipengeleMaelezo
Sifa za KujiungaAlama ya “D” katika Kemia, Baiolojia na somo lolote la tatu
Kozi InayochaguliwaDiploma in Pharmaceutical Sciences
Mfumohttps://www.cas.nacte.go.tz
VyuoMUHAS, CUHAS, St. John, TUDARCo, Mount Meru, n.k
Muda wa MaombiKawaida Juni hadi Septemba kila mwaka

BOFYA HAPA >>> KUPATA ORODHA YA VYUO VINAVYOTOA DIPLOMA YA FAMSI TANZANIA

Bonyeza hapa kuanza > KUTUMA MAOMBO YA CHUO CHA FAMASI ULICHAPENDA KUSOMA

Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *