Masomo ya Diploma ya Famasi Tanzania

Admin

Utangulizi: Orodha Kamili ya Masomo ya Diploma ya Famasi Tanzania – Mwaka wa Kwanza hadi wa Tatu

Taaluma ya famasi ni mhimili muhimu katika sekta ya afya, ikihusisha uzalishaji, usambazaji, matumizi sahihi ya dawa na ushauri wa kitaalamu kwa wagonjwa. Kwa kutambua umuhimu huu, vyuo mbalimbali nchini Tanzania vinatoa kozi ya Diploma ya Famasi chini ya usimamizi wa NACTVET ili kuandaa wataalamu wenye weledi, maadili, na ujuzi wa kati unaohitajika katika mfumo wa afya.

Kozi ya Diploma ya Famasi huchukua muda wa miaka mitatu, ambapo kila mwaka hugawanyika katika Semester I na II. Masomo haya yameundwa kitaalamu ili kumpa mwanafunzi mchanganyiko wa nadharia, mafunzo kwa vitendo (practical), na stadi za kazi (industrial training) zinazohitajika katika mazingira halisi ya kazi.

Katika makala hii, utapata:

  • Orodha ya masomo ya kila mwaka, kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa tatu
  • Mgawanyo wa masomo kwa kila semester
  • Mwanga wa kile unachopaswa kukitarajia kama mwanafunzi wa famasi

Iwe wewe ni mwanafunzi unayetarajia kujiunga, mzazi unayetaka kumsaidia mtoto wako kuchagua kozi sahihi, au mdau wa afya unayetaka kujua mtaala wa elimu ya kati ya famasi nchini – makala hii ni rejea bora na ya kuaminika kwa ajili yako.

MWAKA WA KWANZA
Na.Jina la somoSemester (Mhula)Somo linahusu
1DispensingIUtoaji sahihi wa dawa
2Disease Control and preventionIMagonjwa ya binadamu, matibabu na njia za kuzuia
3Human Anatomy and PhysiologyIMwili wa binadamu ua utendaji kazi wake (seli, Mifupa, Ogani n.k
4Pharmaceutical Dosage FormsIAina za dawa na mifumo yake, jinsi ya kutumia n.k
5Pharmaceutical CalculationsIHesabu za kifamasia, kama vile dose n.k
6Communication SkillsIUjuzi katika mawasiliano
7Basic Computer ApplicationsIUjuzi katika kompyuta
8Laws and Ethics in PharmacyIIMiiko na Maadili katika Taaluma ya Famasi
9Compounding of pharmaceutical liquid preparationsIIJinsi ya kutengeneza dawa za maji
10Pharmaceutical Inorganic ChemistryIIMetali na Simetali na kazi zake katika Ufamasia
11Basic pharmacologyIIMakundi ya dawa, matumizi yake n.k
12Medical Stores KeepingIIJinsi ya kutunza na kupanga dawa eneo la store
13Pharmacy PracticeIIMafunzo kwa vitendo (Field)
MWAKA WA PILI
Na.Jina la somoSemester (Mhula)Somo linahusu
1Medicines and medical supply managementIJinsi ya kutunza kugawa, kununua dawa kwa wazabuni
2Law and policies in PharmacyISheria na sera kwenye famasi
3Pharmaceutical MicrobilogyIWadudu wanaosababisha magonjwa kwa binadamu
4Pharmacology and TherapeuticsIMakundi ya dawa Jinsi zinavyofanya kazi mwili n.k
5Rational Use of MedicinesIMatumizi sahihi ya dawa n.k
6Pharmaceutical organic ChemistryIUmhumi wa Organic Compuound  kwenye Famasi, namna ya kugungundua dawa n.k
7Quality assurance of pharmaceutical productsIIUdhibiti wa ubora wa dawa
8 Pharmaceutics theory and compoundingIIJinsi ya kutengeneza dawa za mafuta (za kupakaa)
9Health information ManagementIIUtunzaji wa taarifa za Afya
10Basic pharmacognosyIIMimea tiba na magonjwa yake, Namna ya kutengeneza
11Pharmacy PracticeIIMafunzo kwa vitendo (Field)
MWAKA WA TATU
Na.Jina la somoSemester (Mhula)Somo linahusu
1Leadership and ManagementIUongozi katika nyanja mbalimbali
2Counselling and Guidance skillsIUjuzi katika kumshauri mgonjwa kwenye hali mbali mbali
3Pharmaceutical ProductionIJinsi ya kutengeneza dawa za vidonge kiwandani
4Health and Medicines PolicyISera za Afya na Dawa
5Health FinancingIMifumo ulipia wa huduma za afya, Bima n.k
6Basic PharmacotherapyIMatibu ya Magonjwa kwa kutumia dawa, namna ya kuchagua dawa sahihi
7Basic Veterinary pharmacologyIDawa baadhi zinatumika kwa wanyama wafugwao
8Pharmaceutical Public HealthIIUteteaji na uchocheaji wa kuboresha afya ya jamii
9EntrepreneurshipIIUjasiriamali katika Famasi
10Operational ResearchIIKufanya utafiti katika sekata za Afya
11Monitoring and Evaluation of Medicines UseIIUfauatiliaji wa matumizi ya dawa, jinsi dawa inavyotengezwa mpaka kufukia jamii
12Pharmacy PracticeIIMafunzo kwa vitendo (Field)

Mapendezo ya Mhuriri;

Hitimisho!

Kozi ya Diploma ya Famasi Tanzania imeundwa kwa umakini mkubwa ili kuwajengea wanafunzi msingi imara wa kitaaluma na vitendo katika taaluma ya afya. Kupitia orodha hii ya masomo iliyopangwa kwa kila mwaka na kila semester, wanafunzi wanapata mwanga wa kile wanachotarajia kujifunza, hali inayowawezesha kuwa na maandalizi mazuri ya kitaaluma na kisaikolojia.

Uelewa wa muundo wa masomo haya si tu unasaidia katika kupanga ratiba za kujisomea, bali pia huwasaidia wanafunzi kujiwekea malengo ya muda mfupi na mrefu katika taaluma yao ya famasi. Hii pia ni nyenzo muhimu kwa wazazi, walezi, na mashirika ya elimu kutathmini ubora na umakini wa mitaala inayotolewa na vyuo vinavyotoa kozi hii.

Ikiwa unalenga kuingia katika sekta ya afya kwa ngazi ya kati, Diploma ya Famasi ni miongoni mwa kozi zenye fursa pana za ajira na maendeleo ya kitaaluma. Hakikisha unafanya maamuzi sahihi mapema, ukianza kwa kuielewa kozi yako kuanzia msingi – kama ulivyojifunza kupitia makala hii.

Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *