Utangulizi
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetoa rasmi ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2025. Ratiba hii inawaongoza wanafunzi wote wa kidato cha nne nchini Tanzania kuhusu siku, muda na masomo yatakayoandikwa kuanzia Novemba 10 hadi Novemba 28, 2025.
Ratiba hii ni nyenzo muhimu kwa watahiniwa, walimu na wazazi kwani inasaidia kupanga muda wa kujisomea na maandalizi ya mwisho kabla ya mtihani.
Muhimu Kabla ya Mtihani
- Watahiniwa wafike mapema kituoni angalau saa moja kabla ya mtihani kuanza.
- Hakikisha unaleta karatasi ya kujibia, kalamu, penseli, ruler, eraser, calculator (kwa masomo yanayohitaji), na vyombo maalum vya practical.
- Hairuhusiwi kuingia na simu, vitabu au maandiko yoyote kwenye chumba cha mtihani.
- Fuata masharti yote ya NECTA Examination Rules and Regulations.
Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2025 (Muhtasari)
Wiki ya Kwanza (10 – 14 Novemba 2025)
- 10/11/2025 – Civics (asubuhi), Biology 1 (mchana)
- 11/11/2025 – Basic Mathematics (asubuhi), Kiswahili (mchana)
- 12/11/2025 – Geography (asubuhi), English Language (mchana)
- 13/11/2025 – Biology 2A Practical (asubuhi), Fine Art 1 (mchana)
- 14/11/2025 – Chemistry 1 (asubuhi), History (mchana)
Wiki ya Pili (17 – 21 Novemba 2025)
- 17/11/2025 – Physics 1 / Engineering Science (asubuhi), Agriculture / Chinese / Textiles (mchana)
- 18/11/2025 – Chemistry 2A Practical (asubuhi), Literature in English & Add Math (mchana)
- 19/11/2025 – Physics 2A Practical, Building Construction, Engineering Drawing (asubuhi), Book Keeping & Electronics Draughting (mchana)
- 20/11/2025 – Biology 2B Practical, Music 1 (asubuhi), Commerce & Engineering subjects (mchana)
- 21/11/2025 – Bible Knowledge & Islamic Knowledge (asubuhi), Arabic & Theatre Arts (mchana)
Wiki ya Tatu (24 – 28 Novemba 2025)
- 24/11/2025 – Fine Art 2, Physics 2B Practical, Textiles Practical (asubuhi), Computer Studies (mchana)
- 25/11/2025 – French Language, Chemistry 2B Practical (asubuhi), Architectural Draughting & Automotive Engineering (mchana)
- 26/11/2025 – Music 2, Biology 2C Practical, Food & Nutrition (asubuhi), Physical Education (mchana)
- 27/11/2025 – Chemistry 2C Practical, Computer Studies 2 Practical (asubuhi)
- 28/11/2025 – Physics 2C Practical, Agriculture 2 Practical (asubuhi)
Pakua Ratiba Rasmi ya PDF
Wanafunzi wanaweza kupakua ratiba kamili ya NECTA kupitia tovuti ya NECTA:
Pakua Ratiba Rasmi ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2025 (PDF)
Ushauri wa Mwisho kwa Watahiniwa
- Tumia ratiba hii kupanga ratiba yako ya masomo nyumbani.
- Fanya mazoezi ya mitihani ya nyuma (past papers) ili kujiamini zaidi.
- Panga muda mzuri wa kulala na kuepuka msongo wa mawazo.
- Omba msaada wa walimu kwa maswali magumu kabla ya siku ya mtihani.

