Vyuo Vinavyotoa Diploma ya Famasi Tanzania – Fursa ya Kitaaluma na Ajira
Katika dunia ya sasa, taaluma ya famasi si tu kuhusu kugawa dawa, bali ni sehemu muhimu ya mfumo wa afya unaohitaji weledi, uadilifu, na maarifa ya kisayansi. Tanzania ikiwa na ongezeko la mahitaji ya wataalamu wa afya, vyuo mbalimbali nchini vimeanzisha kozi ya Diploma ya Famasi (Pharmaceutical Sciences) ili kukidhi hitaji hilo.
Kozi hii huwapa wanafunzi maarifa ya msingi kuhusu dawa, utengenezaji wake, usambazaji, matumizi sahihi, na ushauri kwa wagonjwa – ikiwajengea msingi thabiti wa kitaaluma na kijamii. Kwa wahitimu wa kidato cha nne wanaotamani kuingia kwenye sekta ya afya kwa ngazi ya kati, diploma ya famasi ni chaguo sahihi na lenye matarajio makubwa ya ajira ndani na nje ya nchi.
Katika makala hii, utajifunza kuhusu:
- Orodha ya vyuo vya serikali na binafsi vinavyotoa Diploma ya Famasi nchini Tanzania
- Sifa za kujiunga
- Namna ya kutuma maombi
Ikiwa unatafuta fursa ya kitaaluma yenye mwelekeo mzuri wa ajira, basi endelea kusoma – huenda hapa ndipo mwanzo wa safari yako ya mafanikio katika sekta ya afya.
Orodha ya Vyuo 36 Vinavyotoa kozi ya diploma ya Famasi Tanzania.
S/N | Jina la Taasisi ya Mafunzo | Mkoa | Umiliki |
1 | Muhimbili University of Health and Allied Sciences | Dar es Salaam | Serikali |
2 | Catholic University of Health and Allied Sciences | Dar es Salaam | Serikali |
3 | St. John’s University of Tanzania | Njombe | Binafsi |
4 | City College of Health and Allied Sciences | Dodoma | Binafsi |
5 | Kilimanjaro School of Pharmacy | Kilimanjaro | Binafsi |
6 | Ruaha University College | Iringa | Binafsi |
7 | Royal Training Institute | Mbeya | Binafsi |
8 | St. Peters College of Health Science | Dar es Salaam | Binafsi |
9 | Kampala International University | Dar es Salaam | Binafsi |
10 | Njombe Health Training Institute | Njombe | Binafsi |
11 | St. John College of Health Science | Mbeya | Binafsi |
12 | Spring Institute of Business and Health Science | Dar es Salaam | Binafsi |
13 | University of Dodoma (UDOM) | Dodoma | Serikali |
14 | Tandabui Health College | Mwanza | Binafsi |
15 | Kigamboni City College | Dar es Salaam | Binafsi |
16 | Paradigm Pharmacy College | Dar es Salaam | Binafsi |
17 | Kahama College of Health Sciences | Kahama | Binafsi |
18 | St. Joseph University in Tanzania | Dar es Salaam | Binafsi |
19 | St. Fransic University of Health and Allied Sciences | Ifaranka | Binafsi |
20 | Mtwara Clinical Officer Training Center | Mtwara | Serikali |
21 | St. Maximillian Colbe Health College | Tabora | Binafsi |
22 | DECCA College of Health and Allied Sciences | Dodoma | Binafsi |
23 | St. Aggrey College | Mbeya | Binafsi |
24 | Musoma Utalii College | Tabora | Binafsi |
25 | Blue Pharma College of Health Sciences | Singida | Binafsi |
26 | Apple Valley College of Health Sciences | Dar es Salaam | Binafsi |
27 | Top One College | Songea | Binafsi |
28 | K’s Royal Training Institution | Mbeya | Binafsi |
29 | Green Bird College | Kilimanjaro | Binafsi |
30 | Karagwe Institute of Health and Allied Sciences | Karagwe | Binafsi |
31 | West Tanganyika College | Kigoma | Binafsi |
32 | Mbeya College of Health Sciences | Mbeya | Serikali |
33 | Lugarawa Health Training Institute | Njombe | Binafsi |
34 | Northern College of Health and Allied Sciences | Kilimanjaro | Binafsi |
35 | Peramiho Institute of Health and allied sciences | Ruvuma | Binafsi |
36 | Marian University College (Mar) | Pwani | Binafsi |
SOMA PIA >>> ORODHA YA VYUO VIKUU TANZANIA HAPA
Sifa kujiunga Diploma ya Famasi Nchini Tanzania
Sifa za msingi (kwa CSEE/Kidato cha Nne):
- Ufaulu katika masomo manne yasiyo za dini
- Angalau alama ya “D” katika Kemia na Baiolojia
- Alama ya “D” katika matatu yasioyodini, Aidha ufaulu katika somo the kingereza na hisabati inakupa sifa za ziada za kuendelea kusoma shahada siku za usoni
Jinsi ya Kutuma Maombi ya Diploma ya Famasi Kupitia Mfumo wa CAS – NACTVET
Mfumo wa CAS (Central Admission System) unaosimamiwa na NACTVET hutumika na waombaji wanaotaka kujiunga na vyuo vya afya, mafundi sanifu, ualimu wa diploma, n.k. kwa ngazi ya Certificate (Astashahada) na Diploma (Stashahada).
1. Tembelea Tovuti Rasmi ya CAS – NACTVET
- Fungua tovuti ya CAS kwa kiungo: https://www.cas.nacte.go.tz
2. Bonyeza Sehemu ya “Start Application” au “New Applicant”
- Kwa mara ya kwanza, jisajili kwa kutumia:
- Jina lako kamili
- Email ya kuaminika
- Namba ya simu
- Nambari ya mtihani wa NECTA (CSEE)
- Baada ya kujisajili, utapata jina la mtumiaji (username) na neno la siri (password)
3. Ingia kwenye Akaunti Yako
- Tumia username na password kuingia kwenye akaunti
- Mfumo utaonesha taarifa zako za NECTA (kwa waliomaliza kidato cha nne)
- Hakikisha taarifa zote ni sahihi
4. Chagua Kozi ya Kuomba – Diploma ya Famasi
- Katika menyu ya kozi, tafuta “Diploma in Pharmaceutical Sciences”
- Chagua chuo/vyuo vinavyotoa kozi hiyo
- Unaweza kuchagua hadi vyuo vitano (5) tofauti
5. Jaza Taarifa Zilizobaki
- Taarifa binafsi: tarehe ya kuzaliwa, makazi, jinsia
- Pakia picha ya pasipoti (passport size)
- Hakikisha kila sehemu umejaza ipasavyo
6. Lipa Ada ya Maombi (Application Fee)
- Ada ni TSh 10,000
- Mfumo utakupa control number
- Lipa kupitia:
- M-Pesa / Tigo Pesa / Airtel Money
- Benki ya NMB, CRDB, au benki nyingine
Mfano wa Kulipa kwa M-Pesa:
Piga
*150*00#
→ LIPA kwa M-Pesa → Malipo ya Serikali → Ingiza control number → Kiasi → Namba ya siri
7. Thibitisha na Tuma Maombi
- Baada ya kulipa, nenda tena kwenye akaunti yako ya CAS
- Hakikisha taarifa zote ni sahihi
- Thibitisha (Submit) maombi yako
8. Subiri Majibu ya Uchaguzi
- Orodha ya waliochaguliwa hutangazwa kupitia:
- Akaunti yako ya CAS
- Tovuti ya NACTVET
- Simu (SMS) au barua pepe
- Ukichaguliwa, utapata Joining Instructions kutoka chuo husika