Matokeo ya Kidato cha Sita 2025/2026 – NECTA Form Six Results 2025/26Tanzania

Haya hapa Matokeo Kidato cha Sita 2025 NECTA Form Six Results 2025/2026

Taarifa Muhimu Kuhusu Matokeo ya Kidato cha Sita 2025

Wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita mwezi Mei–Juni 2025 wanapaswa kufuatilia kwa karibu tangazo hili kupitia tovuti rasmi ya NECTA na vyanzo vingine vya habari.

Ufaulu wa Kidato cha Sita 2025 Wafikia Asilimia 99.95 – Watahiniwa 71 Wafutiwa Matokeo

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza kuwa ufaulu wa jumla katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwaka 2025 umefikia asilimia 99.95. Kati ya watahiniwa 126,135 waliofanya mtihani huo, ni asilimia 0.03 zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita — jambo linaloashiria ongezeko dogo lakini chanya katika viwango vya ufaulu kitaifa.

Mtazamo wa Mwandishi: Ushauri Muhimu Baada ya Matokeo ya Kidato cha Sita 2025

Tahadhari Muhimu kwa Wanafunzi wa Kidato cha Sita 2025: Usichelewe Kutuma Maombi ya Chuo

Kama mtaalamu wa masuala ya udahili tangu mwaka 2017, napenda kutoa tahadhari kwa vijana wote waliomaliza Kidato cha Sita mwaka huu. Taarifa za matokeo zinaonyesha kuwa kiwango cha ufaulu mwaka 2025 kimepanda kwa kiwango cha juu, jambo linalotarajiwa kuongeza ushindani mkubwa katika nafasi za kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.

Hii inaweza kuwa changamoto, lakini pia ni fursa kwa wale watakaojiandaa mapema.
Usisubiri dirisha la udahili lifunguliwe ndipo uanze kutafakari chuo na kozi unazotaka kuomba.

Kwa Wenye Ufaulu wa Kati au Wa Kawaida

Ni muhimu mapema kuchagua kozi zinazolingana na alama zako ili kuongeza nafasi ya kupokelewa.
Kumbuka, baadhi ya kozi maarufu hujaa haraka hata kabla ya awamu ya kwanza kumalizika.

Kwa Wenye Ufaulu wa Juu

Usidharau ushindani.
Hata kama ufaulu wako ni mzuri, bado vyuo hutumia utaratibu wa kujaza nafasi kulingana na muda wa maombi na ushindani wa kozi husika.
Maombi ya mapema huongeza uwezekano wa kupata kozi na chuo unachopendelea.

Kumbuka:
Kila mwaka, wanafunzi wengi wanakosa nafasi ya chuo si kwa sababu hawakufaulu, bali kwa sababu walichelewa kutuma maombi.
Usirudie kosa la wengine — andaa nyaraka zako sasa na uwe tayari kuomba mara tu dirisha litakapofunguliwa..

Tembelea Makala Zetu za Udahili

Kwa msaada zaidi kuhusu jinsi ya kujiunga na vyuo, vigezo vya kozi, na muda sahihi wa kutuma maombi, tembelea makala zifuatazo:

Hata hivyo, NECTA imethibitisha kuwa watahiniwa 71 wamefutiwa matokeo yao kwa sababu mbalimbali zikiwemo udanganyifu katika mitihani na ukiukwaji wa kanuni za mitihani. Baraza limeeleza kuwa hatua hizi ni sehemu ya kulinda uadilifu na usawa katika mfumo wa elimu nchini.

Kwa ujumla, matokeo haya yanaonyesha maendeleo endelevu katika sekta ya elimu, huku NECTA ikiendelea kuimarisha usimamizi na teknolojia ya upimaji wa wanafunzi nchini.

Tarehe za Muhimu (ACSEE 2025)

TukioTarehe
Mtihani wa Kidato cha SitaMei – Juni 2025
Matokeo Kutangazwa na NECTAJulai 7, 2025 (Imethibitishwa Yametoka)
Dirisha la Mikopo HESLBJuni – Agosti-septemba 2025
Maombi ya Vyuo kupitia TCUJulai – Agosti 2025

Jinsi ya Kuangalia Matokeo Kidato cha Sita

NECTA hutoa matokeo kupitia njia mbalimbali kwa urahisi wa wanafunzi wote:

1. Kupitia Tovuti ya NECTA

  • Bofya sehemu iliyoandikwa “Results”
  • Chagua ACSEE (Advanced Certificate of Secondary Education Examination)
  • Chagua mwaka 2025
  • Tafuta jina la shule
  • Tafuta namba ya mtahiniwa (form six index number)
    Mfano: S0334/0021/2025
    Mwisho → utaona orodha ya namba za watahiniwa na alama zao.

2. Linki ya Moja kwa Moja

3. Jinsi ya Kuangalia Matokeo yako Kwa USSD (Hatua zote muhimu)

Njia ya USSD ni bora kwa wanafunzi wasio na vifaa vya intaneti:

  1. Piga *152*00#: Fungua sehemu ya kupiga simu kwenye simu yako na piga namba *152*00#.
  2. Chagua “Elimu”: Kutoka kwenye menyu inayojitokeza, chagua namba inayohusiana na “Elimu”.
  3. Chagua “NECTA”: Katika menyu inayofuata, chagua “NECTA”.
  4. Kisha, chagua “Matokeo”.
  5. Chagua “ACSEE”: Chagua aina ya mtihani, yaani, “ACSEE” kwa Kidato cha Sita tu.
  6. Ingiza Namba ya Mtihani na Mwaka: Andika namba yako ya mtihani,  mfano, S0001-0222-2025
  7. Pokea Matokeo: Subiri baada ya kukamilisha malipo, utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo yako. Huduma hii inaweza kupatikana kwa Gharama Tshs 100/= kwa kila SMS

Madaraja ya Ufaulu kwa Kidato cha Sita (ACSEE) Tanzania

A. Uainishaji wa Madaraja kwa Jumla ya Pointi (Division)

DarajaJumla ya Pointi (Masomo 3)Maelezo
Daraja la Kwanza (I)3 – 9Ufaulu wa juu sana
Daraja la Pili (II)10 – 12Ufaulu wa juu
Daraja la Tatu (III)13 – 15Ufaulu wa kati
Daraja la Nne (IV)16 – 18Ufaulu wa chini
Daraja Sifuri (0)19 – 21Hajahitimu (amefeli)

Mfano: Mwanafunzi aliyepata C, C, D atakuwa na pointi 3+3+4 = 10, hivyo Daraja la Pili.

B. Alama za Somo Moja na Pointi Zake

Ufafanuzi wa Alama za Kidato cha Sita (NECTA – ACSEE)

AlamaWastani wa Alama (%)Maana
A80 – 100Bora Sana (Excellent)
B70 – 79Vizuri Sana (Very Good)
C60 – 69Vizuri (Good)
D50 – 59Wastani (Satisfactory)
E40 – 49Inaridhisha (Moderate)
S35 – 39Daraja la Ziada (Subsidiary Pass)
F0 – 34Haujafaulu (Fail)

Alama ya “S” hutumika kwa somo la ziada (General Studies) na haitumiki kwenye hesabu ya division.

Kumbuka Muhimu:

  • Ufaulu wa mwanafunzi hupimwa kupitia masomo matatu ya tahasusi (combination subjects).
  • General Studies hupewa alama yake lakini haihesabiwi kwenye jumla ya pointi za division.
  • Alama ya F katika masomo matatu ya msingi humaanisha mwanafunzi amefeli (Division 0).

Hatua za Kufanya Baada ya Matokeo

Baada ya kupata matokeo yako:

1. Tafuta Kozi Unayopenda

2. Omba Mkopo HESLB

3. Jisajili kwa Maombi ya Vyuo Vikuu

  • Tumia mfumo wa TCU (CAS) kuomba vyuo zaidi ya kimoja.

4. Pata Ushauri wa Taaluma

  • Wasiliana na walimu, wazazi, au washauri wa elimu kabla ya kuchagua kozi.

Orodha ya Mikoa na Shule Maarufu kwa Matokeo

Kwa urahisi zaidi, unaweza kutazama matokeo kulingana na shule au mkoa:

  • Dar es Salaam
  • Dodoma
  • Arusha
  • Mbeya
  • Mwanza
  • Tanga

Mapendekezo ya Mhariri;

Hitimisho

Matokeo Kidato cha Sita ni hatua ya mwisho kabla ya mwanafunzi kujiunga na elimu ya juu. Ni muhimu kujua alama zako, kuchagua kozi kwa uangalifu, na kuanza haraka mchakato wa maombi ya vyuo na mikopo. Endelea kutembelea tovuti yetu kwa taarifa zote muhimu, updates, na mwongozo sahihi wa safari yako ya kitaaluma.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

    Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *