Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2025 – Taarifa Muhimu kwa Wazazi na Wanafunzi!
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuinua viwango vya elimu nchini likiwa linaangazia kutangaza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita (ACSEE) kwa mwaka 2025.
Mtihani huu ni hatua ya mwisho ya elimu ya sekondari, na matokeo yake huwa ni msingi wa kuamua ni wanafunzi gani watapata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu, vyuo vikuu, au fursa nyingine za kitaaluma na kijamii.
Katika makala hii, tutakuletea muhtasari wa matokeo hayo, shule zilizofanya vizuri, tahasusi zilizoongoza, pamoja na jinsi ya kuangalia matokeo rasmi kupitia tovuti ya NECTA Katika makala hii, tutakupa mwongozo kamili wa jinsi ya kuangalia matokeo yako, kuelewa mfumo wa madaraja, na hatua za kuchukua baada ya kupata matokeo yako.
Hii ni taarifa muhimu kwa wazazi, wanafunzi, walimu, na wadau wote wa elimu. Endelea kusoma ili kufahamu kwa undani kila kitu kuhusu ACSEE 2025.
Ni lini Matokeo Zinatarajiwa Kutolewa?
- Matokeo ya ACSEE kwa mwaka 2025 yanatarajiwa kutolewa mapema Julai 2025. Hii ni kwa sababu matokeo ya A‑Level huyaachiwa mapema—mnamo mwaka 2022 yalitolewa tarehe Jumatatu, Julai 5, 2022, na utaratibu huo unatarajiwa kuendelea mwaka huu, hivyo tunaatara kutangazwa kati ya kati tarehe 1 mpaka 15 Julai mwaka 2025.
- Wanafunzi hushauriwa kuziangalia taarifa rasmi za NECTA mara kwa mara ili kuhakikisha hawakosei upatikanaji wa matokeo yao.
- Matokeo yatakuwa ya wazi kwa wanafunzi kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao rasmi ya mtihani NECTA na njia za kidigitali kama USSD.
Alama na Madaraja Yaliyotumika Katika Mitihani ya Kidato cha Sita 2025
Uelewa wa alama na madaraja ni muhimu kwa wanafunzi na wazazi kuelewa kiwango cha ufaulu. List lifuatalo linaonyesha maana ya madaraja na alama katika mtihani wa kidato cha sita 2025.
- A: Alama 80-100: Maana yake ni (Bora Sana)
- B: Alama 70-79: Maana yake ni (Vizuri Sana)
- C: Alama 60-69: Maana yake ni (Vizuri)
- D: Alama 50-59: Maana yake ni (Wastani)
- E: Alama 40-49: Maana yake ni (Inaridhisha)
- S: Alama 35-39: Maana yake ni (Daraja la Ziada)
- F: Alama 0-34 Maana yake ni (Haujafaulu)
Madaraja ya ufualu yanayotumika kidato cha sita
Madaraja ya ufaulu kwa Kidato cha Sita (yaani, matokeo ya mtihani wa mwisho wa elimu ya sekondari ya juu — ACSEE) nchini Tanzania hupangwa kwa kuzingatia wastani wa pointi (Division Points) kutoka kwenye masomo matatu ya tahasusi aliyosoma mwanafunzi. Haya ndiyo madaraja:
- Daraja la Kwanza (Division I) – Pointi 3 hadi 9
- Daraja la Pili (Division II) – Pointi 10 hadi 12
- Daraja la Tatu (Division III) – Pointi 13 hadi 15
- Daraja la Nne (Division IV) – Pointi 16 hadi 18
- Daraja Sifuri (Division O) – Pointi 19 hadi 21
Kumbuka:
- Kila daraja la ufaulu kwenye somo moja hupewa pointi kulingana na alama:
- A = 1, B = 2, C = 3, D = 4, E = 5, S = 6, F = 0 (Haijapita)
Njia Tatu (3) Rahisi za Kupata Matokeo ya Kidato cha Sita 2025
Kupata matokeo ya kidato cha sita ni rahisi sana, mchakato huu umekuzwa kwa matumizi ya teknolojia ya kisasa. Njia tatu rahisi ni:
- Kupitia Tovuti Rasmi ya NECTA
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA (https://www.necta.go.tz)
- Ingiza namba yako ya mtihani pamoja na kanuni za usalama.
- Kupitia Njia ya USSD
- Tumia simu yako ya mkononi, ingiza nambari 15201#
- Fuata maelekezo na ingiza namba yako ya mtihani.
- Kupitia Shule au Vyuo
- Tembelea ofisi za shule au vyuo ulivyosoma.
- Mwalimu au msimamizi wa mtihani atakutoa matokeo.
Ni Wapi Naweza Kupata Matokeo Kidato cha Sita?
- Tovuti rasmi ya NECTA (www.necta.go.tz)
- Kwenye Tovuti yetu: (www.bongoportal.com/)
- Huduma za USSD kupitia simu za mkononi
- Mashirika ya habari kama redio, televisheni na magazeti
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita Mtandaoni (Hatua kwa Hatua)
Kufuatilia matokeo yako mtandaoni ni rahisi ukifuata hatua hizi:
- Fungua kivinjari (browser) kwenye simu, kompyuta au tablet yako.
- Andika au bofya: www.necta.go.tz, kisha ingia kwenye tovuti rasmi ya NECTA.
- Ukifikia ukurasa wa NECTA, bofya kwenye tab au menyu inayoitwa “Results”. Chagua “ACSEE” (Kidato cha Sita).
- Subiri ukurasa mpya uanze kupakia matokeo—hii inaweza kuchukua muda kadri trafiki ya mtandao inavyohamisha data.
- Baada ya kupakia:
- Chagua mwaka (2025),
- Kisha bofya exam centre (kituo cha mtihani au shule yako).
- Wakati wa kuangalia matokeo:
- Tafuta jina la shule yako au “index number” yako.
- Matokeo yako yataonekana kwa muundo wa orodha: viwango (A–E), daraja (Division I–IV/0).
- Chunguza matokeo yako kwa usahihi. Kama umefaulu, unaweza kuchukua screenshot au kuchapisha (“print”) kwa kumbukumbu.
Ufafanuzi wa video jinsi ya kuangalia Matokeo ya Form Six 2025
Inakuja hivi karibuni!
Kiungo cha Kuangalizia Matokeo Kidato cha Sita 2025/2026
Wanafunzi Tanzania wanaweza kupata matokeo yao kupitia kiungo rasmi cha NECTA:
- Tovuti rasmi: www.necta.go.tz
- Kiungo/ Link Matokeo: https://www.necta.go.tz/results/view/acsee
Jinsi ya Kuangalia Matokeo Kidato cha Sita Kwa Njia ya USSD
Njia ya USSD ni bora kwa wanafunzi wasio na vifaa vya intaneti:
- Piga *152*00#: Fungua sehemu ya kupiga simu kwenye simu yako na piga namba *152*00#.
- Chagua “Elimu”: Kutoka kwenye menyu inayojitokeza, chagua namba inayohusiana na “Elimu”.
- Chagua “NECTA”: Katika menyu inayofuata, chagua “NECTA”.
- Kisha, chagua “Matokeo”.
- Chagua “ACSEE”: Chagua aina ya mtihani, yaani, “ACSEE” kwa Kidato cha Sita tu.
- Ingiza Namba ya Mtihani na Mwaka: Andika namba yako ya mtihani, mfano, S0001-0222-2025
- Pokea Matokeo: Subiri baada ya kukamilisha malipo, utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo yako. Huduma hii inaweza kupatikana kwa Gharama Tshs 100/= kwa kila SMS
Hitimisho;
Matokeo Kidato cha Sita 2025 ni hatua muhimu katika safari ya elimu ya mwanafunzi nchini Tanzania. Ufaulu katika mtihani huu hufungua milango ya kujiunga na vyuo vikuu, taasisi za elimu ya juu, na fursa nyingine za kitaaluma. Kwa wale ambao matokeo yao hayakufikia matarajio, ni muhimu kukumbuka kuwa mafanikio ya maisha hayategemei mtihani mmoja pekee; kuna njia nyingi za kufikia malengo yako.
Kwa taarifa zaidi na kuangalia matokeo yako, tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.necta.go.tz au piga *152*00# kisha fuata maelekezo.
Tunawatakia heri wanafunzi wote katika hatua inayofuata ya maisha yao ya kitaaluma na kijamii. Matokeo haya ni mwanzo mpya wa safari ya mafanikio.