Fahamu kalenda kamili ya TCU 2025 kwa ajili ya udahili wa wanafunzi wa shahada ya kwanza, pamoja na mzunguko wa maombi, majibu ya waliochaguliwa, na muda wa kuthibitisha kozi.
Utangulizi
Kila mwaka, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) hutangaza rasmi kalenda ya udahili kwa shahada ya kwanza kwa wanafunzi wa Tanzania na kutoka nje ya nchi.
Kwa mwaka 2025/2026, kalenda hii inaonyesha tarehe rasmi za:
- Kuanzia kwa udahili
- Kila mzunguko (round ya 1 hadi ya 4)
- Muda wa kuthibitisha (confirmation)
- Tarehe za kutangaza waliochaguliwa (selected applicants)
Ni muhimu kwa mwanafunzi kufuata ratiba hii kwa ukamilifu ili kuhakikisha hakosi fursa ya kujiunga na chuo anachotamani.
Kalenda ya Maombi ya Udahili wa Vyuo Vikuu 2025 (TCU Official Calendar)
Mzunguko | Tarehe ya Kuanzia | Tarehe ya Mwisho | Maelezo |
---|---|---|---|
Mzunguko wa Kwanza (Round I) | 17 Juni 2025 | 15 Agosti 2025 | Wanafunzi wanatuma maombi kwa mara ya kwanza |
Kuthibitisha waliochaguliwa | 10 – 22 Agosti 2025 | Kupitia account yako! | |
Mzunguko wa Pili (Round II) | 23 Agosti 2025 | 31 Agosti 2025 | Kwa waliokosa chuo au kubadilisha chuo |
Kuthibitisha waliochaguliwa | 27 – 30 Agosti 2025 | Kwa waliopata nafasi mpya | |
Mzunguko wa Tatu (Round III) | 2 – 10 Septemba 2025 | Nafasi za ziada au kuchagua upya | |
Mzunguko wa Mwisho (Wa Nne) | 15 – 25 Septemba 2025 | Fursa ya mwisho ya maombi | |
Wanachuo kuwasili Chuoni | Kuanzia Oktoba 2025 | Chuo husika kitaelekeza |
Muhimu Kujua:
- Maombi yote ya vyuo hufanyika kupitia mifumo ya vyuo vyenyewe (sio kwenye tovuti ya TCU).
- Mwanafunzi hapaswi kuomba zaidi ya kozi tatu kwa chuo kimoja.
- Kuthibitisha kozi ni hatua ya lazima ili kukubaliwa rasmi chuoni.
- TCU system ni sehemu ambayo mwanafunzi anaweza kuona:
- Vyuo alivyopata
- Kuthibitisha chuo kimoja (kwa kutumia special code)
Mfumo wa CAS (TCU Central Admission System)
Ili kufanikisha mchakato wa udahili, TCU hutumia mfumo wa pamoja wa udahili kwa shahada ya kwanza ujulikanao kama.
Hatua za Kufuata:
- Tembelea tovuti ya chuo unachotaka (mf. UDOM, SUA, UDSM)
- Fuata link ya “Apply Now” au “Online Application”
- Jisajili kwa taarifa zako sahihi
- Lipa ada ya maombi kupitia control number
- Chagua kozi (programmes) hadi 3
- Thibitisha chuo kupitia TCU confirmation code ukipata nafasi
Tahadhari kwa Waombaji
- Tumia taarifa sahihi za kitaaluma (NECTA form four & six index numbers)
- Usitumie majina yasiyolingana na vyeti
- Thibitisha mara moja baada ya kuchaguliwa – ukikosa, nafasi huenda kwa mwingine
- Usichelewe kuomba – round ya kwanza huwa na ushindani mdogo zaidi
- Epuka kutuma maombi kwa simu – tumia laptop/computer unapoweza
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
Je, naweza kuomba vyuo zaidi ya kimoja?
Ndiyo, unaweza kuomba vyuo tofauti kadhaa, lakini unathibitisha kimoja tu ukichaguliwa.
Maombi ya HESLB yataendana na udahili?
Ndio. Dirisha la HESLB hufunguliwa kuendana na ratiba ya TCU round I.
Nini nikifanye nikikosa chuo katika round ya kwanza?
Tumia round ya pili kuomba tena au kubadilisha kozi.
Naweza kubadilisha kozi/chuo?
Ndiyo, kwa kutumia mfumo wa round nyingine, unaweza kufanya mabadiliko.
Viungo Muhimu:
Hitimisho
Kwa mwanafunzi anayetarajia kujiunga na chuo kikuu mwaka 2025/2026, ratiba hii ya TCU ni mwongozo wako muhimu zaidi. Hakikisha unafuata kwa umakini kila tarehe, unaomba mapema, na unathibitisha nafasi yako haraka.
Jitayarishe, chagua kwa umakini, na usichelewe!