Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2025 (Selection Form Five 2025-2026)- TAMISEMI

Admin

Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2025 : Mwongozo Kamili wa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo ni huu hapa!

Makala hii itakuongoza hatua kwa hatua kupata orodh ya waliochaguliwa kidato ch tano na vyuo vya ufundi,  Na rahisi soma kwa Makini Makala hii.

  • Umechaguliwa kwenye orodha rasmi ya TAMISEMI? Hongera sana kwa mafanikio yako! Hii ni fursa ya kukuza elimu yako na kujiandaa kwa changamoto za elimu ya juu zaidi.
  • Lakini, je, unajua hatua zote muhimu za kuchukua baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo?
  • Je, unajua jinsi ya kuangalia orodha ya waliochaguliwa kwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi?, kupata fomu, na hatua za kujiunga?

TAMISEMI leo imechapisha taarifa rasmi kupuitia ukurasa wake ikisema leo  tarehe 6 juni 2025 itatoa “Taarifa kuhusu Uchaguzi wa Wanafunzi kidato cha tano na Vyuo vya Ufundi”

Kujiunga na Kidato cha Tano ni hatua muhimu sana kwa kila mwanafunzi anayetaka kuendelea na elimu ya sekondari na hatimaye kufanikisha ndoto zao za kitaaluma ya kujiunga na vyuo vikuu ndani na nje ya Tanzania.

Ni lini TAMISEMI inatangaza Orodha ya Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2025?

  • Orodha ya Waliochaguliwa kidato cha tano 2025/26 imetanganza  leo 06 Juni 2025.

Ni Wanafunzi wangapi wamechaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo 2025?

Hata hivyo, kwa mwaka uliopita wa 2024, jumla ya wanafunzi 188,787 walichaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati. Kati yao, 131,986 walipangiwa shule za sekondari, na 56,801 walipangiwa vyuo vya elimu ya ufundi.

Ni wapi orodha wa waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na vyuo vya ufundi inapatikana?

Viungo (Linki) za kuangalia waliochagliwa kidato cha tano Mtandaoni 

  • Tovuti rasmi ya Selform TAMISEMI (https://selform.tamisemi.go.tz/)
  • Kiungo mama: https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/2025/first-selection/index.html

Jedwali la mikoa la kuangalizia Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo Vya Ufundi 2025

(CHAGUA “MKOA” ULIOSOMA KUONA  JINA LAKO KWENYE 

ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

Jinsi ya kuangalia selection za form five 2025 na vyuo vya kati

Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI: https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/ 

  1. Tafuta kiungo cha “Orodha ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025” au (First Selection Form Five, 2025).
  2. Chagua “MKOA” uliosoma.
  3. Chagua “HALMASHAURI YA WILAYA” uliosoma.
  4. Tazama“JINA LA SHULE” uliosoma kwenye orodha.
  5. Sasa anagalia na uhakiki kama Jina lako ni mmojawapo kwenye orodha

Mfano: Kama umechaguliwa kidato cha tano, jina lako litakuwa kwenye orodha ya shule husika.

NB: Tunakukumbusha kuangalia taarifa muhimu za uchaguzi waki kama Vile;

  • Kwa wanafunzi Waliochaguliwa kidato cha Tano 2025;
  1. Jina la shule uliyopangiwa,
  2. Mkoa ambao shule inapatikana
  3. Masomo uliyopangiwa maarufu kama “KOMBI – Form Five Combination” mfano; PCM, PCB, HGL, EGM, CBG, n.k
  • Kwa wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vya Ufundi 2025;
    1. Jina la chuo
    2. Mkoa inapopatikana
    3. Kozi ulipangiwa
    4. Ada ya chuo husika pia inapatikana miongoni mwa hizo taarifa

Mapendekezo Ya Mhariri:

Vigezo Vilivyotumiwa na TAMISEMI Kuchagua Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Vyuo 2025

Katika mchakato huu wa uchaguzi, TAMISEMI hutumia vigezo vya haki na usawa kwa kuzingatia:

  • Matokeo Wanafunzi ya kidato cha nne 2024 yaani CSEE
  • Machaguo ya Mwanafunzi aliyopendekeza kwenye selform yake.
  • Wanafunzi wenye sifa zinazolingana na vigezo vya shule husika.
  • Uhakiki wa taarifa za wasaidizi wa shule, wazazi na mamlaka za elimu.
  • Watu wenye uhitaji maalumu kama walemavu n.k

Hatua Muhimu Baada ya Kufahamika Kuwa umechaguliwa kidato cha tano

  • Hakikisha umewasiliana na viongozi wa shule ulichaguliwa kupitia mawasilio ya simu yaliyopo kwenye fomu ya Kujiunga
  • Jiandae kwa ajili ya masomo kwa kununua vitabu na vifaa vingine, ikiwemo sare ya shule au chuo husika.
  • Pata taarifa kuhusu tarehe ya kuanza masomo.
  • Shiriki mafunzo ya awali (tuisheni) kama yanapatikana hasa kwa Wanafunzi Waliochaguliwa masomo ya sayansi kwani huwa yana vitu vingi vya kujifunza
  • Ulizia miongozo kuhusu utawala wa shule na ratiba za masomo.

Kupitia hatua hizi, utaweza kuhakikisha unajitayarisha kwa mafanikio ya kidato cha tano.

Ufaulu wa kidato cha nne wa mwaka jana ulivyoongeza joto za uchaguzi kidato cha tano an vyuo

  • Ufaulu wa kidato cha nne wa mwaka jana ulivyoongeza hisia za uchaguzi kidato cha tano an vyuo 2025
  • Ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2024 umeongezeka kwa asilimia 3, kutoka asilimia 89.36 mwaka 2023 hadi asilimia 92.37 mwaka 2024.
  • Hii inaashiria kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walifaulu na hivyo kuhitaji nafasi zaidi katika kidato cha tano na vyuo vya kati

Ongezeko hili la ufaulu linaweza kuathiri mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano kwa njia zifuatazo:

  1. Upatikanaji wa Nafasi: Kwa kuwa idadi ya wanafunzi waliofaulu imeongezeka, kunaweza kuwa na ushindani mkubwa kwa nafasi chache zilizopo katika shule za sekondari na vyuo vya kati.
  2. Uchambuzi wa Matokeo: TAMISEMI inaweza kuchukua muda zaidi kuchambua matokeo na kupanga wanafunzi katika shule na vyuo mbalimbali kulingana na ufaulu wao.
  3. Marekebisho ya Miundombinu: Serikali inaweza kuhitaji kufanya marekebisho ya miundombinu ya shule na vyuo ili kukidhi ongezeko la wanafunzi.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu uchaguzi kidato cha tano na Vyuo;

  1. Je, nitafanyaje kama sijachaguliwa?

Unaweza kutuma maombi kwenye shule binafsi au kutafuta njia mbadala kama Kujiunga na Elimu ya Ufundi au Vyuo vya Kati kutoka sekta binafsi.

  1. Ni lini masomo ya kidato cha tano na vyuo huanza?

Kwa kawaida masomo huanza kawaida mwezi Julai kwa wafunzi wa kidato cha tano na mwezi September kwa waliochaliwa vyuo vya kati.

  1. Ninapokeaje fomu ya kujiunga?

Fomu hupatikana shule husika au mtandao wa TAMISEMI pamoja na vituo vya elimu (shuleni au chuoni)

Hitimisho

Kwa kuhitimisha, orodha ya waliochaguliwa kidato cha tano 2025 ni fursa ya dhahabu kwa wanafunzi walioendelea na masomo ya kidato cha tano (Form Five) na Vyuo vya kati vya ufundi.

Jiandae kwa uangalifu, fuata hatua zilizoainishwa kwenye jedwali na hakikisha unafuata utaratibu wa kujiunga.

Ukitimiza hili kwa makini, utakuwa katika mstari wa mbele wa mafanikio yako ya elimu.

Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *