UTANGULIZI
City College of Health and Allied Sciences (CCHAS) ni moja kati ya vyuo bora vya afya nchini Tanzania vinavyotoa kozi mbalimbali za ngazi ya Cheti (Certificate), Diploma, na baadhi Degree katika fani za afya na Maendeleo ya jamii.
Kwa mwaka wa masomo 2025/2026, chuo kimefungua rasmi dirisha la maombi ya udahili, ambapo wanafunzi wanaotaka kusomea afya wanaweza kuomba kupitia mfumo wa mtandaoni au moja kwa moja chuoni.
KOZI ZINAZOTOLEWA CCHAS
Hizi ni baadhi ya kozi maarufu zinazotolewa:
Ngazi ya Kozi | Kozi Inayopatikana | Muda wa Masomo |
---|---|---|
Cheti (NTA Level 4) | Basic Technician Certificate in Nursing | 1 mwaka |
Diploma (NTA Level 6) | Ordinary Diploma in Nursing and Midwifery | 3 miaka |
Cheti | Pharmaceutical Sciences | 1 mwaka |
Diploma | Medical Laboratory Sciences | 3 miaka |
Diploma | Clinical Medicine | 3 miaka |
Kozi nyingine zinaweza kubadilika kulingana na kibali cha NACTVET. Hakikisha unaangalia tangazo rasmi la chuo.
SIFA ZA KUJIUNGA
Kwa Cheti:
- Awe amemaliza Kidato cha Nne (Form IV)
- Awe na angalau alama ya D katika masomo ya Sayansi (Biology, Chemistry, Physics)
- Awe na Uwezo wa Kusoma na Kuandika Kiswahili & Kiingereza
Kwa Diploma:
- Awe amemaliza Kidato cha nne (Form IV) au Cheti cha Afya kinachotambulika na NACTVET (NTA Level 5)
- Awe na alama nzuri kwenye masomo ya Sayansi
- Awe amepata nafasi kupitia NACTVET Admission System au direct application
JINSI YA KUOMBA UDAHILI CHUO CHA CITY COLLEGE (ONLINE)
Njia 1: Kupitia Mfumo wa Udahili wa NACTVET
- Tembelea: https://www.nacte.go.tz
- Fungua mfumo wa Central Admission System (CAS)
- Tafuta “City College of Health and Allied Sciences”
- Chagua kozi unayotaka
- Jaza taarifa zako binafsi, elimu, na nyaraka muhimu
- Lipia ada ya maombi (10,000 TZS)
- Hakikisha unahifadhi control number na form yako
Mapendekezo ya Mhariri;
- Kozi za afya za diploma zenye mkopo
- Kozi afya zenye soko kubwa la ajira
- Matokeo ya Kidato cha Sita 2025
- Mwongozi Kamili wa Kuomba Mkopo wa Wanafunzi 2025
- Jinsi ya kuomba (Kutuma) Maombi) Mkopo ya Mkopo HESLB 2025
- Mwisho wa Kutuma Maombi ya Mkopo 2025
- Dirisha Maombi ya mkopo Elimu ya Juu 2025
- Jinsi ya Kutuma Maombi UDSM
TAREHE (MUDA) WA MAOMBI YA CHUO CHA CITY COLLEGE
- Dirisha la Maombi: Mei 27 hadi 11 Julani 2025 (Awamu ya Kwanza)
- Muda wa mwisho kutuma maombi: Angalau Septemba 30, 2025
- Mafunzo Kuanza: Oktoba au Novemba 2025
NYARAKA ZINAZOHITAJIKA
- Cheti cha kuzaliwa
- Vyeti vya elimu (Form IV)
- Picha 3 za pasipoti (passport size)
- Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA
MAWASILIANO YA CHUO (City College of Health and Allied Sciences)
HITIMISHO
City College of Health and Allied Sciences (CCHAS) ni chuo bora kwa wale wanaotaka taaluma za afya zenye ajira ya uhakika. Hakikisha unaanza mchakato wa maombi mapema, unaandaa nyaraka zote muhimu, na unaweka taarifa zako sahihi. Kumbuka: Afya ni maisha, elimu ni msingi wa mafanikio.